Kelele hazina mzoefu au mgeni, wote kwa pamoja hatupendi kelele kwenye mipango na biashara zetu.
Hatua ya kwanza ya kutathimini ushauri ni kuangalia umetoka kwa nani. Mrejesho wa kuupa uzito ni ule unaotoka kwa watu wanaojali unachokifanya na wanapenda ukue.   

Hasidi ni mtu ambaye huweka lawama, lugha chafu, asiyekupa nafasi ya kumuelewesha.

Kwenye biashara Hasidi hutoka sehemu yoyote ile, sio kila mtu hufurahi wewe unapoanzisha jambo lako.Kuwepo kwa hasidi kwenye biashara yako hilo sio tatizo, tatizo litakua pale unapotaka kumfurahisha hasidi, hapo ndipo hupelekea baadhi ya watu kufunga biashara zao.

Hasidi haridhiki, kama ambavyo Hasidi hana sababu.

Ni muhimu sana unapoletewa maoni au malalamiko kujua kuwa ni malalamiko yenye picha ipi.
Sio kila mrejesho wa kushughulika nao kwa nguvu sawa, wapo wanaotoa malalamiko kusudi ili kukukatisha na safari yako ya biashara.