Matangazo pekee sio msaada kama haujali wateja.

https://www.waziriconcept.com/2020/02/matangazo-pekee-sio-msaada-kama-watoa.html
Kwenye kukuza soko kila njia inaukomo wake. Tangazo la Tv au redio litafanya utambulike kuwa upo na kuwashawishi wateja kwa mara ya kwanza au kuwakumbusha walioanza kukusahau, lakini matangazo hayo hayatakupa uhakika kuwa wateja hao wataendelea kubaki kwakua kazi ya tangazo sio kubakisha mteja.

Mteja aweze kubaki na kujiona yupo sehemu sahihi inahitajika juhudi zaidi ya kuchapa tangazo na kubandika barabarani kwani hilo kila mtu analiweza.

1.Hakikisha unatimiza kama ulivyo ahidi.
Ingawa sio muda wote tunasema ukweli kwenye biashara, lakini yakupasa ujue sehemu zipi hazitaki uongo kwenye biashara. Boresha Maisha yako kwa kutumia bidhaa zetu, Ingawa sio kweli mteja baada ya kununua bidhaa yako Maisha yake yatakua bora lakini hatokuita muongo. Pata punguzo la asilimia 50 kwa kununua bidhaa 3, mteja kajitutumua kanunua kweli bidhaa 3 kisha punguzo unatoa asilimia 20 hapo atakuita muongo.

2.Kubali na kukiri kosa pale unapoona umemkosea mteja au wafanyakazi wako.
Kukubali kosa ni jambo linalowapendeza sana wateja. lakini kukubali huko kunapaswa kuendane na mabadiliko kwenye lile ulilokosea. Bidhaa umezalisha chini ya kiwango, toa tamko na urekebishe. Mteja umemjibu lugha isiyofaa, omba radhi na urekebishe, fanya hivyo hivyo unapowakosea wafanyakazi na wasaidizi wako.


Ingawa sio muda wote tunasema ukweli kwenye biashara, lakini yakupasa ujue sehemu zipi hazitaki uongo kwenye biashara.


3.Lengo la biashara ni faida lakini usioneshe wazi kwa mteja.
Kweli tunanjaa ya mafanikio lakini hilo linatakiwa kuishia kwako na wafanyakazi wako na sio kwa wateja ambao wanakuja kwako kutatua matatizo yao. Onyesha huruma inapotakiwa kuoneshwa, kuwa rafiki kwao kuliko kuwa muuzaji tu. Hili ni pamoja na kukubali hasara kwa lengo la kumbakisha mteja kwa ajili ya kesho. Wateja watakupenda na hawatatamani kuhama kwako.